PICHA 6: Benz za umeme watakazopewa Leicester na bilionea baada ya kushinda Kombe la EPL


Wachezaji wa klabu ya Leicester City ambao wameisaidia klabu hiyo kuingia katika historia isiyofutika ya kutwaa taji la Ligi Kuu
Uingereza kwa mara kwanza toka ianzishwe miaka 132 iliyopita, tayari wameanza kupokea zawadi za pongezi kwa kuweka rekodi hiyo, lakini kubwa ni bilionea Vichai Srivaddhanaprabha kutangaza kuwapa zawadi ya Mercedes B-Class Electric Drive.



Mercedes B-Class Electric Drive ni gari ya umeme yenye thamani ya pound 32,670 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 100 za kitanzania, kiasi ambacho kwa wachezaji 30 watakuwa wamemgharimu Vichai Srivaddhanaprabha pound milioni 1 ambazo ni zaidi ya bilioni 3 za kibongo.


Hata hivyo kabla ya kutangaza kutoa zawadi hiyo Vichai Srivaddhanaprabha aliwahaidi wachezaji wa Leicester City kwenda kuenjoy kwa pamoja historia ya kutwaa taji hilo Las Vegas Marekani, gharama zote akizigharamia yeye.





Related Posts:

0 Response to " PICHA 6: Benz za umeme watakazopewa Leicester na bilionea baada ya kushinda Kombe la EPL"

Post a Comment